Amkeni mifupa mitupu
Pokeeni hewa (Nani nani)
Mifupa mikavu
Valishwa misuli (Atakayesimama)
Ni nani nani atakayepaza
Sauti ya haki?
Nena bubu nena
Kumejaa ukorofi
(Chorus)
Nani,nani?
Atakayesimama
Atakayehesabiwa
Nani, nani?
Lazaro! Lazaro!
Fufuka Lazaro
Ondoa jiwe kaburini
Vua nguo za kifo
Tetea mjane
Mume wake amekatwa shingo
Na nyundo ya haki imwemwangukia kichwa
(Chorus)
(Bridge)
Kondoo upande wa kuume
Mbuzi upande wa kushoto
Kondoo upande wa kuume
(Chorus)




