Tuchezecheze kama mwali wa moto
Tusongesonge kama miti kwa upepo
Wimbo wetu unaimbwa kwenye redio
Songa karibu nikusikie ukipumua
(Chorus)
Miili yetu yakigusana hio ni sawa
Nimefika peponi
Moyo umeruka
Aii,wewe mchumba
Fungua pazia tazama nje
Mng’aro wa mataa ya mji ukumulike
Kivuli chako ni kama picha
Ningelikuwa msanii ningekuchora
(Chorus)
Ngozi yako ni kama Hariri
Ukiniruhusu nitakubusu
Utamu wako haupimiki
Kiuno chako chanipunguza nguvu




