Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero
Umewahi kuangalia huko chini(aye aye)
Mtu maskini akiiba mkate
Atavalishwa pingu miaka minne
Lakini tajiri anayezorotesha umaskini wa nchi nzima (mwajijua)
Anachekacheka na hakimu
Baadaye wapo wote pamoja mikahawani
(Chorus)
Dunia ina mambo
Kweli ina mambo
Dunia ina mambo
Dunia ina mambo
Nyuma ya kila mlango/Vituko na vichekesho/mbele ya kila wazo
Dunia ina mambo
Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero
Ni dini gani inayoendeleza chuki (mambo bado)
Kwa ajili ya bidii ya bin adam
Mimi sina kazi
Warumi wachukia wakristo wengine
Wengine wachukia Waislamu (bure bilash)
Waislamu wachukia Wayahudi
Na nguvu zangu zote singeweza hayo yote
(Chorus)
Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero
Ni kulala mnalala au vipi (hallo hallo)
Mnaruhusu viongozi wa nchi tajiri
Kumiliki nchi masikini
Kwa mfano wananchi wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni
Waliporwa mali zao au siyo (au siyo)
Basi mbona walionyanyaswa wasipande ndege
Na kwenda ng’ambo ili kurudisha haki zao
(Chorus)




