VERSE 1
Hebu shika maarifa
Kama wewe mgeni mjini huu wa taifa
Hizo pesa ufiche
Na huo mzigo uushike
Unapofika huko kibanda
Cha Akamba usikawie
Wenyeji wa Nairobi hawafiki mjini
Usiku wa manane
CHORUS
Wasiojua wanapewa ujuzi
Wasiojua
Wanaowinda huamka jioni
Wanaowinda
VERSE 2
Hebu shika maarifa
Kama we mwenye gari mjini huu wa taifa
Mtokaa ikikwama lazima ujue utachota
Msaada wa bure huwa na bei
Hasa ikiwa Friday
Usiwanyime pesa zao za pombe
Usiku wa manane
CHORUS
Wasiojua wanapewa ujuzi
Wasiojua
Wanaowinda huamka jioni
Wanaowinda
PRE-CHORUS
Na usifike huko mtaani
Kama ujulikani
Utauwacha mshahara wa mwezi
Usiku wa manane
CHORUS
Wasiojua wanapewa ujuzi
Wasiojua
Wanaowinda huamka jioni
Wanaowinda




