VERSE 1
Mzee alisema hakuna cha bure
Huo msemo tumeutafsiri kinyume
Hata shule kuingiza mtoto
Lazima utoe mchoto
Kupata simu ni balaa
Road license bei nafuu untanunua
Kupoteza ID ni mashaka
Twarudhisha jamhuri yetu nyuma
CHORUS
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe ndugu
Nenda Limuru
VERSE 2
Hata nyumbani ukipatwa na majambazi
Kupiga 9-9 wasema, ‘Sisi hatuna gari.
Lete elfu tano ya petroli.
Saidia utumishi.’
Mahakamani pesa ndio haki
Kwa elfu chache mshtakiwa ndiye mshtaki
Utajiri huwa ushahidi
Twarudisha jamhuri yetu nyuma jamani
CHORUS
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka soda e Inspekta
Burudika na Fanta
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe Mama
Nunua Ketepa
VERSE 3
Huko Kenyatta madawa zimeisha
Mashiti zauzwa marikiti mia kwa mia
Wafanyi kazi waenda miezi bila pesa
Ni bahati ukitibiwa
Mzigi wetu unazidi kuwa mzito
Watoto wanne na mshahara ya elfu mbili mia tano
Ya vitabu, na viatu, na vyakula
Nauliza na Mbotela
Je huu ni ungwana
CHORUS
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe ndugu
Nenda Limuru
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe Mama
Nunua Ketepa




