VERSE 1
Umoja ni fahari yetu
Undugu ndiyo nguvu
Chuki na ukabila
Hatutaki hata kamwe
Lazima tuungane
Tuijenge nchi yetu
Pasiwe hata mmoja
Anayetenganisha
CHORUS
Naishi, natumaini, najitolea daima Kenya
Hakika ya bendera ni uthabiti wangu
Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
Daimi mimi
Mwananchi mzalendo
VERSE 2
Kwa uchungu na mateso
Kwa vilio na huzuni
Tulinyakuliwa huzuni
Na mashujaa wa zamani
Hawakustushwa na risasi
Au kufungwa gerezani
Nia yao ukombozi
Kuvunja pingu za ukoloni
CHORUS
BRIDGE
Wajibu wetu ni kuishi kwa upendo
Kutoka ziwa mpaka pwani
Kaskazini na kusini
CHORUS




