VERSE 1
Jana bus stesheni
Nimechoka kwenye laini
Kijana mmoja anikaribia na cassetti
Eti, ‘Chief nunua mziki.
Olomide spesheli,’
Kuisikiza kamwuliza
‘Hii lugha gani, hii?’
‘Trouser, longi, mufuto
Paka nyau pussy
Bosolo-we, bosolo-you, bosolo-me’
Siku iliyofuata nikamtafuta mwenye cassetti
Kumwuliza tafadhali ajibu swali
CHORUS
Bolingo na ngai
Humaanisha vipi nikikuuliza utasema nini eee
Dombolo na ngai
Twalipia maneno matamu au matusi ooo
VERSE 2
Natembea huku mjini na hewa mfokoni
Napanda ‘23’ ya Kangemi
Dereva aongeza sauti
Kama sisi ni viziwi
Ni wimbo wangu umepatikana kichinichini
‘Nasikitika nambari uliyopiga
Haitumiki kwa sasa e
Tafadhali jaribu tena baadaye’
Nani atinilinda
Wapi sheria
Simama nikuone Bwana Minista
CHORUS
BRIDGE
Nunueni Okatch Biggy
Nunueni Kabaselleh
Nunueni Princess Jully
Nunueni ya wenyeji
Panda Panda!
Panda!
Panda Panda!
Panda!
Panda Panda!
Panda!
Sisi sote tupande
Bolingo na ngai
Bolingo na ngai
Ndombolo na ngai
Ndombolo na ngai




